Poractant alfa
Poractant alfa, inayouzwa kwa jina la chapa Curosurf na mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia matatizo ya kupumua (RDS) kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.[1][2] Inapunguza hatari ya kifo na hali ya hewa kuingia kwenye sehemu kati ya mapafu na kuta za kifua (pneumothoraces).[2] Inatolewa kwenye njia ya hewa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mapigo ya moyo ya polepole, shinikizo la chini la damu na oksijeni ya chini.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuziba kwa mrija wa ndani ya njia ya hewa (endotracheal tube).[1] Dawa hii inaundwa na surfactant ya mapafu ambayo ina phospholipids na protini za surfactant.[1]
Dawa hii iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1999.[1] Nchini Marekani, iligharimu takriban dola 1,000 za Marekani kwa mililita 3 kufikia mwaka wa 2021.[3] Imetengenezwa kutoka kwa mapafu ya nguruwe.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Poractant Alfa Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "DailyMed - CUROSURF- poractant alfa suspension". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Curosurf Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)